If I Must Die...

Kama lazima nife

Translated to Swahili by

Kama lazima nife

Lazima uishi

Kwa kusimulia hadithi yangu

Kwa kuuza vitu vyangu

Kwa kununua kipande cha nguo

Na vidwe vichache

(Fanya kiwe cheupe, chenye mkia mrefu)

Ili mtoto, mahali gani katika Gaza,

Pale akitazama mbinguni

Akingojea babake aliyeondoka katika moto--

Na hakumuaga mtu

Hata si nyama yake

Hata si mwenyewe--

Aone mwewe, mwewe wangu ulioujenga, utaporuka juu juu

Na ili afikirie kwa kitambo kidogo kwamba malaika apo

Kwa kuleta upendo

Kama lazima nife

Iwe ni hadithi


Select poem translation

A poem by Refaat Alareer.